Ali

Mturuki huyu aliyekuwa amefungwa na kifungo cha ulevi alimwona Isa al Masih kwenye ndoto na maisha yake yakabadilika daima. Japokuwa alikata tamaa, alihamia Saudi Arabia, mahali ambapo kileo kimekatazwa. Hata hivyo alipofika, aliona vinywaji vikali pale. Hivyo akafanya safari kwenda Mekka, akitumaini kuwa atakuwa huru na kuondokana na mazoea mabaya ya kuzoelea pombe na kwamba atakuwa amebadilika na kuongozwa kwenye njia ya kweli ya kiislamu. Kilichomshangaza ni kwamba badala yake alikutana na Isa al Masih mwenyewe!