Ndoto na Maono kuhusu Isa al Masih

Shuhuda tano zilizotukuka au kusifika sana kwa miongo kadhaa sasa, mambo ya ajabu au vitendo vya kushangaza sana, vimekuwa vikijirudia rudia ulimwenguni, hasa katika nchi za kiislamu. Wanaume kwa wanawake - na hata bila kuifahamu injili na hata bila kuwa na mawasiliano yoyote na Wakristo - wamejikuta wanabadilisha maisha yao, yaani mabadiliko ya milele baada ya wao kuwa na ndoto au maono ya Isa al Masih. Ripoti nyingi za matukio haya ya miujiza yamekuwa yakitokea mara nyingi huko katika nchi zilizojiwekea mkazo katika msimamo mkali wa kidini. Nchi ambazo kuhubiri injili kumekatazwa na kupigwa marufuku kabisa, mahali ambapo ikiwa mtu fulani angebadili dini yake na kuwa Mristo, kwa sheria yao angehukumiwa kifo!

Hali inayojitokeza na kukubalika kwa wote ni kuwa ndoto huwajia watu wale wote wanaotafuta kumjua na kumpendeza Mungu. Tuliamua kuchukua baadhi ya matukio yaliyowahi kutokea, na kuvitumia hapa kama kitu cha ushahidi kwa waislamu ulimwenguni kote.

Masimulizi ya Maisha halisi

Kwa kupitia mahojiano ya ana kwa ana na watu mbalimbali, tumeweza kuchagua maelezo ya maisha halisi ya watu ambao walikuwa waislamu zamani na kisha wakamfahamu Isa kama Bwana na Mwokozi wao. Toka mwanzoni, mtengenezaji amefanya kila jitihada kuwakilisha Uislamu kama ulivyo tofauti katika nchi mbalimbali duniani kote. Na kwa ajili ya sababu hiyo habari hizi zilichaguliwa kutoka Misri, Iran, Uturuki, Nigeria na Indonesia. Kila moja ya masimulizi haya ya “Zaidi ya Ndoto” limetengenezwa katika lugha yake ya asili katika muundo wa tamthilia fupi na kwa kunaswa kwa picha za video zenye ubora. Filamu hii inaambatana na sehemu ya huduma inayoelezea vizuri jinsi ya kumfuata Isa al Masih na kuwaongoza watazamaji kwenye sala ya wokovu.