Dini

Binti wa kiindonesia aliyedhalilishwa na familia yake, marafiki na jamii kwa jumla, kwa sababu aliuacha Uislamu na kuokoka yaani kumfuata Isa al Masih na kuwa mfuasi wa Isa al Masih usiku ule wa LAILATUL QADAR usiku ambao waislamu humpelekea maombi yao Allah, na ndio usiku ule ule ambao Isa al Masih mwenyewe alimtokea katika maono. Kutoka wakati ule alipomwona Isa al Masih, amani ya Isa al Masih ilimjaa moyoni mwake na kukaa naye hata ule wakati ambapo alikuwa akipitia mateso au kuudhiwa kwa ajili ya uamuzi huo.