Khosrow

Kijana wa Iran, akiwa amevunjika moyo na kukosa matumaini kabisa, alikutana na Isa al Masih katika maono. Mwokozi alimnyoshea mikono na kumwambia amshike, akimwahidi kuwa "maisha yako yatabadilika milele." Aliishika mikono ya Isa al Masih, akawa anaelezea hivi: "Mawimbi kama nguvu za umeme zilipita mwilini mwangu tena na tena. Nililia sana kwa mara nyingine tena tangu nilipokuwa mtoto mdogo na furaha ya ajabu ilijaa moyoni mwangu."