Mohammed

Mtu wa kabila la Wafulani aliyekuwa akichunga wanyama huko Nigeria aliupata upendo wa kina na utawala wa Isa al Masih kupitia mfululizo wa ndoto kadhaa za ajabu. Mabadiliko katika maisha ya Mohamedi yametokea kwa jinsi Isa alivyomtokea katika ndoto zote. Ingawa baba yake alijaribu kumwua wakati alipokata shauri kumfuata Isa, alinusurika mara kwa mara alipotishiwa maisha yake na hatimaye akamwongoza baba yake kwenye imani ndani ya Isa al Masih.