Shuhuda tano za ajabu

Khalil kutoka Misri.

Khalil

Mtu mwenye ukatili hata tungeweza kumwita gaidi, alibadilika kutoka kuwa mwuaji "Sauli" na kuwa mtu aliyeweza kusamehe wengine "Paulo" baada ya kutembelewa na Isa al Masih kwa ndoto iliyomwingia moyoni mwake. Mtu huyu aliyekuwa amewachukia Wakristo hata na Wayahudi, alipanga mpango wa kuidhalilisha Injili. Hatimaye badala yake yeye mwenyewe alibadilishwa kabisa wakati ule Isa al Masih alipomtokea na kubadilisha moyo wake.
⟩ Soma zaidi

Mohammed mtu wa kabila la Wafulani kutoka Nigeria

Mohammed

Mtu wa kabila la Wafulani aliyekuwa akichunga wanyama huko Nigeria aliupata upendo wa kina na utawala wa Isa al Masih kupitia mfululizo wa ndoto kadhaa za ajabu. Mabadiliko katika maisha ya Mohamedi yametokea kwa jinsi Isa alivyomtokea katika ndoto zote. Ingawa baba yake alijaribu kumwua wakati alipokata shauri kumfuata Isa, alinusurika mara kwa mara alipotishiwa maisha yake na hatimaye akamwongoza baba yake kwenye imani ndani ya Isa.
⟩ Soma zaidi

Binti wa kiindonesia aliyedhalilishwa na familia yake.

Dini

Binti wa kiindonesia aliyedhalilishwa na familia yake, marafiki na jamii kwa jumla, kwa sababu aliuacha Uislamu na kuokoka yaani kumfuata Isa al Masih na kuwa mfuasi wa Isa al Masih usiku ule wa LAILATUL QADAR usiku ambao waislamu humpelekea maombi yao Allah, na ndio usiku ule ule ambao Isa al Masih mwenyewe alimtokea katika maono. Kutoka wakati ule alipomwona Isa al Masih, amani ya Isa al Masih ilimjaa moyoni mwake na kukaa naye hata ule wakati ambapo alikuwa akipitia mateso au kuudhiwa kwa ajili ya uamuzi huo. ... ⟩ Soma zaidi

Mturuki Ali alimwona Isa kwenye ndoto na maisha yake yakabadilika daima.

Ali

Mturuki huyu aliyekuwa amefungwa na kifungo cha ulevi alimwona Isa al Masih kwenye ndoto na maisha yake yakabadilika daima. Japokuwa alikata tamaa, alihamia Saudi Arabia, mahali ambapo kileo kimekatazwa. Hata hivyo alipofika, aliona vinywaji vikali pale. Hivyo akafanya safari kwenda Mekka, akitumaini kuwa atakuwa huru na kuondokana na mazoea mabaya ya kuzoelea pombe na kwamba atakuwa amebadilika na kuongozwa kwenye njia ya kweli ya kiislamu. Kilichomshangaza ni kwamba badala yake alikutana na Isa al Masih mwenyewe! ... ⟩ Soma zaidi

Khosrow kutoka Iran amevunjika moyo na kukosa matumaini kabisa.

Khosrow

Kijana wa Iran, akiwa amevunjika moyo na kukosa matumaini kabisa, alikutana na Isa al Masih katika maono. Mwokozi alimnyoshea mikono na kumwambia amshike, akimwahidi kuwa "maisha yako yatabadilika milele." Aliishika mikono ya Isa al Masih, akawa anaelezea hivi: "Mawimbi kama nguvu za umeme zilipita mwilini mwangu tena na tena. Nililia sana kwa mara nyingine tena tangu nilipokuwa mtoto mdogo na furaha ya ajabu ilijaa moyoni mwangu." ⟩ Soma zaidi

Ndoto zilizotoka kwa Isa al Masih. Watu wamejikuta wanabadilisha maisha yao, yaani mabadiliko ya milele baada ya wao kuwa na ndoto au maono ya Isa al Masih.

Ndoto zilizotoka kwa Isa al Masih

Watu wakiwa kwenye njia panda maishani - hua na kilia moyoni, wakitaka kumuelewa Mungu kindani zaidi. Inasemekana ya kwamba, ndani ya moyo wa kila mwanadamu, kuna pengo ambalo tu Mungu ndiye anayeweza kulijaza. Kwenye hadithi hizi tano za kweli ambazo zimekusanywa kutoka sehemu mbali mbali duniani, utakutana na wato ambao walikumbana na pengo hilo na kujiweka kwenye hatari ya kupoteza yote ili kulijaza pengo hilo na ukweli. Walitafuta na kugundua zaidi ya mazingaombwe, zaidi ya uchawi, zaidi ya tambika, zaidi ya dini, zaidi ya ndoto.